Ulimwengu azidi kupiga hatua

Saturday , 2nd Dec , 2017

Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amezidi kupiga hatua za kurejea dimbani kutokana na kuendelea vizuri na mazoezi ya kujiweka sawa.

Ulimwengu anayekipiga katika klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden yuko katika mazoezi makali ya Gym, kuchezea mpira peke yake na mkufunzi pamoja na kukimbia ufukweni.

Mshambuliaji huyo alifanyiwa upasuaji wa goti katika hospitali ya Taasisi ya Sayansi ya Michezo mjini Cape Town, Afrika Kusini mapema mwezi Julai baada ya kusumbuliwa kwa mrefu na majeraha ya goti.

Ulimwengu hajafanikiwa kuitumikia kikamilifu timu yake mpya ya AFC Eskilstuna  tangu alipojiungana nayo mwezi Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).