Mbao FC
Kwa mujibu wa pande hizo mbili ni kwamba pesa hiyo itakuwa ikiongezeka kama timu hiyo itaendelea kufanya vyema katika michezo yake ya ligi hiyo.
Na hapa wawakilishi wa Hawaii Meneja Masoko, Erisalia Ndeta na Mwenyekiti wa Mbao FC ya Mwanza, Solly Zephania Njashi wamezungumzia udhamini huo na kusema kuwa utakuwa na manufaa katika klabu hiyo, na ligi kiujumla, pia utakuwa ni chachu ya kuiongezea makali klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.