Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Habari wa BMT, Najaha Bakari amesema uchaguzi huo umekuwa ukisua sua kutokana na wagombea kushindwa kuchukua fomu za ugombea kwa muda uliopangwa suala linalochangia uchaguzi huo kuahirishwa kwa mara ya tatu sasa.
Najaha amesema, mchezo huo upo nyuma sana tofauti na michezo mingine suala linalochangia pia watu kushindwa kujitokeza pia kuzingatia kuwa wachezaji wengi wa mchezo huu ni watu kutoka nchini India.