Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema, ili kuwa mwenyeji wa michuano hiyo unatakiwa kuwa na timu bora kwani kama wenyeji timu itaingia moja kwa moja katika hatua za makundi.
Kizuguto amesema, programu ya vijana hao imeshaanza na Juni mwaka huu kutakuwa na michuano ya chini ya miaka 13 itakayofanyika mkoani Mwanza kwa kushirikisha mikoa yote ambapo makocha watapata nafasi ya kuchagua vijana wenye vipaji watakaoweza kuunda timu ya Taifa itakayoshiriki michuano hiyo ya mwaka 2019.