Ijumaa , 11th Nov , 2016

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Wanawake ‘Twiga Stars’ jana Novemba 10, 2016 ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji Cameroon kwa kupigwa mabao 2-0 na sasa inajipanga kulipiza kisasi katika mchezo wao wa pili, Nov 13

Twiga Stars

 

Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Sebastian Nkoma amesema: “Nimeona upungufu katika mchezo wa jana, nafanyia kazi.”

Bao la kwanza katika mchezo wa jana lilifungwa na Mshambuliaji Ngoya Ajara wa Klabu ya Sundsvalls ya Sweden ambaye pia ndiye Mchezaji Bora wa mwaka 2016 nchini Cameroon wakati bao la pili lilifungwa na Kiungo wa Klabu ya Aurillac ya Ufaransa Ngono Mani Michelle katika dakika ya 71.

Twiga Stars wao wamealikwa na Waandaaji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016 – Cameroon ambao wameamua kuipa heshima Tanzania na kuona kuwa timu hiyo ina ubora wa na kwamba inafaa kuipimana ubavu kabla ya kuanza kwa fainali hizo Novemba 19, mwaka huu.

Kikosi cha Twiga Stars wamo makipa, Fatma Omari na Najiat Abbas; mabeki ni Wema Richard, Sophia Mwasikili, Anastasia Katunzi, Maimuna Hamisi, Fatuma Issa, Happiness Mwaipaja na Mary Masatu wakati viungo ni Donisia Minja, Stumai Abdallah, Amina Ally, Anna Mwaisura na Fadila Kigarawa ilhali washambuliaji ni Fatuma Swalehe, Asha Rashid na Mwanahamisi Omari.

Kikosi cha Cameroon