Jumanne , 31st Dec , 2019

Leo ni siku ya mwisho kwa mwaka 2019, tunayakumbuka matukio makubwa yaliyojiri katika tasnia ya michezo, ambapo EATV, EA Radio na mitandao yake ya kijamii leo inakuchambulia matukio hayo mwaka huu.

Matukio ya kimichezo mwaka 2019

Kenye tasnia ya masumbwi mwaka 2019 umekuwa mzuri, yakifanyika marekebisho ya sheria za vyama vinavyoongoza mchezo huo pamoja na kuendelea kukua kwa mabondia wengi nchini. Mfano mkubwa ni Hassan Mwakinyo ambaye amecheza mapambano mawili makubwa, likiwemo lile alilocheza dhidi ya Arnel Tinampay wa Ufilipino.

Zifuatazo ni baadhi ya tweets zinazoonesha matukio makubwa yaliotokea katika michezo kwa mwaka 2019.

Tukio lingine ambalo halitosahaulika ni rekodi ya nahodha wa Taifa Stars na klabu ya Genk, Mbwana Samatta ambaye katika mwaka 2019 akiwa na klabu yake ya Genk ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya Klabu Bingwa Ulaya na kufunga bao, akifunga jumla ya mabao matatu katika hatua ya makundi ikiwemo Liverpool.