Jumanne , 8th Sep , 2015

Kocha wa Simba SC Dylan Kerr amesema kikosi chake kitafanya vizuri katika msimu ujao wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza Jumamosi kwa kupata ushindi wa 'kihistoria' ugenini itakapokabiliana na wenyeji African Sports uwanja uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Kerr amesema anataka kuona Simba inashinda Jumamosi na kuendeleza rekodi yake ya kushinda mechi ya kwanza ambayo ni muhimu kwa kuijenga timu kwa wachezaji wake mbinu mbalimbali za kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ya kwanza ili wapate nguvu ya kupambana mechi inayofuata.

Kerry amesema, mechi mbili za ugenini ni ngumu, ila wakishinda ya kwanza, inayofuata pia watakuwa wamejipanga zaidi na watawapa hofu wapinzani wao.

Katika kuhakikisha kwamba wamedhamiria kushinda, uongozi wa Simba ulimsafirisha Kerr na msaidizi wake, Suleimani Matola, Jumapili kwenda Tanga kwa lengo la kuipeleleza African Sports ambayo ilikuwa inacheza mechi ya kirafiki na Coastal Union ambapo kikosi cha Simba kimeweka kambi visiwani Zanzibar na kinatarajiwa kuondoka visiwani humo Alhamisi asubuhi kuelekea Tanga tayari kwa mchezo huo utakaofanyika Jumamosi na kubaki jijini humo kuwasubiri Mgambo Shooting hapo Septemba 16 mwaka huu.