Jumapili , 16th Aug , 2015

Nahodha msaidizi wa mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Himid Mao amesema wataichapa Yanga SC kwa mara nyingine watakapokutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Katika taarifa yake, Himid amesema upinzani wa siku za karibuni baina ya klabu hizo mbili ni kutokana na ubora wa klabu hizo kwa sasa na wanaamini watatwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa kufanya hivyo mara tatu mfululizo.

Kwa upande mwingine Azam Fc imeibuka na ushindi wa bao 3-0 katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya Mafunzo ya Zanzibar Uwanja wa Amaan hapo jana ambapo ,mabao ya Azam Fc yalifingwa na mabeki Shomary Kapombe, Aggrey Morris na mshambuliaji na Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’.

Azam FC imeweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 22 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Yanga SC.