Jumatano , 26th Oct , 2016

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub amesema inasikitisha kocha waliyemzoea akiondoka lakini wapo tayari kufanya kazi na kocha mpya

Cannavaro

 

Canavaro amewataka  mashabiki wa timu yao kuwa watulivu na kuondoa wasiwasi kufuatia kujiuzulu kwa kocha wao Mkuu Hans van der Pluijm

Cannavaro amesema, wachezaji wameumizwa na jambo hilo lakini hawana namna ila wapo tayari kufanya kazi na kocha yeyote atakaye pendekezwa na uongozi wao kwa kuwa ndiyo maamuzi yaliyofikiwa.

Tayari, Mzambia George Lwandamina amewasili juzi Dar es Salaam na inadaiwa amekuja kusaini mkataba wa kuchukua nafasi ya Pluijm, jambo ambalo limemkera Mholanzi huyo na kuamua kuondoka.

Hans Van der Pluijm