Jumatatu , 16th Nov , 2015

Timu ya JKT Ruvu inatarajia kusajili wachezaji watatu katika Dirisha Dogo la Usajili la Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara lililofunguliwa hapo jana.

Katibu mkuu wa klabu hiyo Ramadhan Madoeka amesema, lengo la kusajili wachezaji hao ni kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji, beki wa kati na winga.

Madoeka amesema, kocha mkuu wa timu hiyo Abdallah Kibaden amependekeza katika ripoti kuwa anahitaji asajiliwe wachezaji hao kwani idara hizo zinaonesha upungufu mkubwa katika michezo yao ya ligi kuu bara na kushindwa kupata matokeo mazuri.

JKT Ruvu inashika nafasi ya 15 kutokana na pointi tano walizovuna katika michezo 10 ikishinda mmoja, sare mbili na kupoteza michezo saba.