![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2023/08/29/7X9A3133_1000x667-scaled.jpg?itok=pcguCswp×tamp=1693320984)
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Robertinho amesema pamoja na kikosi kufanya vizuri katika mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara, nguvu zimeelekezwa katika michuano ya kimataifa.
“Tunajipanga kuanza michuano ya kimataifa kwa kishindo, lengo ni kufanya vizuri kwa kuvuna alama tatu ugenini, nina imani na kikosi changu,” amesema Robertinho.
Simba SC itaanzia ugenini katika mechi ya kuwania kucheza hatua ya makundi katika mechi itakayofanyika kati ya Septemba 15, 16 mwaka huu. Mchezo marudiano utachezwa kati ya Septemba 29, 30 au Oktoba Mosi, mwaka huu.
Dynamos imefuzu hatua ya pili na kupangwa kucheza na Simba SC baada ya ushindi wa bao 1-0 ikiwa nyumbani katika uwanja wa Levy Mwanawasa, Ndola dhidi dhidi ya African Stars na kupata matokeo ya jumla ya sare ya mabao 2-2.
Simba SC itaanza kampeni ya mashindano ya kimataifa ikiwa na rekodi ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2003, 2018/19, 2020/21 na 2022/23.