
Katibu mkuu wa klabu hiyo Osward Morris amesema, wanaanza mazoezi leo kwa ajili ya maandalizi ya muendelezo wa ligi hiyo.
Morris amesema, wamerudi kujipanga upya ili waweze kufikia malengo yao katika kuhakikisha wanacheza soka la ushindani.
Morris amesema, uongozi wa klabu hiyo unatarajia kukutana leo kwa lengo la kujadili ripoti iliyowasilishwa na kocha wao Salum Mayanga.