
kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars - Kim Paulsen
“kila mtu anafahamu ubora na uimara wa Algeria lakini watu wanapaswa kuelewa pindi ukienda kucheza nao iwe ugenini au nyumbani kitu cha kwanza unapaswa kuwaheshimu kwamba unacheza na timu gani lakini sisi tutaingia uwanjani tukiwaheshimu na tutaenda kupambana nao maana tunajua ni mchezo mgumu na wachezaji wapo tayari kwa mchezo “ - amesema Kim Poulsen
Pia kocha Paulsen amesema kikosi chake kitakosa huduma ya kiungo Himid Mao Mkami anayeuguza majeraha. Taifa stars iko kundi F na timu za Algeria, Uganda na Niger, ambapo katika mchezo wa kwanza Taifa Stars ilitoka sare ya goli moja kwa moja na Niger huku Algeria ikiwalaza Uganda kwa mgaoli mawili kwa sifuri.