Jumatatu , 30th Nov , 2015

Chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania TSA kimesema kina mpango wa kuweka sheria maalum kwa ajili ya kusimamia mchezo wa kuogelea chini.

Katibu Mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka amesema, sheria hizo zitawasaidia waogeleaji kuweza kuelewa kwani Makocha hao watakuwa na elimu pamoja na uelewa wa kutosha tofauti na hivi sasa ilivyo ambapo baadhi ya makocha wanatoa mafunzo kwa waogoleaji kimazoea.

Namkoveka amesema, sheria hizo hazitawagusa makocha peke yake lakini hata waogeleaji walio katika ngazi za vilabu ambao wataweza kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa watatakiwa kuwa katika viwango maalum ambavyo vitawekwa ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.