Jumanne , 13th Aug , 2024

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mafunzo ya siku moja ya mameneja wa klabu Arobaini na nane zinazoshiriki Ligi kuu Tanzania bara pamoja na Ligi ya championship yenye lengo ya kuwafundisha mfumo wa kisasa kuhusu utunzaji wa taarifa kuelekea msimu mpya wa mashindano wa 2024-25

Afisa habari wa bodi ya Ligi(TPLB) Karim Boimanda amesema kuwa washiriki sitini wamepatiwa mafunzo hayo huku TPLB haitosita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu Mameneja wote watakoshindwa kutunza taarifa kuhusu klabu zao ndani ya msimu wa 2024-25.

''Zamani tulikuwa tunatumiwa Line Up ya wachezaji kwa kuandika hivyo Mameneja watakuwa wanajaza huko walipo wakisave sisi watu ambao tunahusika na mfumo huo tutakuwa tunaona'' amesema Boimanda

Kwa upande wao,Baadhi ya mameneja waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo wameeleza jinsi walivyonufaika na mafunzo hayo kuelekea msimu mpya wa mashindano ambapo ligi kuu Tanzania Bara inataraji kuanza Agosti 16-2024.