Mchezo huo ambao unahusisha bingwa mara mbili wa Africa Wydad Casablanca ya Morocco dhidi ya bingwa mara tano wa Africa TP Mazembe utapigwa kwenye uwanja wa Stade Mohammed V, uliopo katikati ya jiji la Casablanca nchini Morocco.
Pambano hilo la 'CAF SUPER CUP' litaanza majira ya saa 1:30 usiku ambapo hadi sasa timu hizo zimeshawahi kukutana mara 4, Wydad Casablanca wakishinda mara 2, na TP Mazembe wakishinda mara 1 na wametoka sare mara 1.
Tayari msimu wa 2017/18 wa michuano hiyo mikubwa Afrika kwa vilabu umeshaanza ambapo Tanzania inawakilishwa na timu ya Yanga kwa upande wa ligi ya mabingwa huku Simba ikiwa katika michuano ya kombe la shirikisho.



