Jumatatu , 24th Nov , 2014

Timu ya Taifa ya wanawake ya Mchezo wa Kriketi inatarajia kuondoka nchini Desemba 12 mwaka huu kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika Desemba 14 mwaka huu.

Akizungumza na Muhtasari wa michezo,Kocha wa atimu hiyo,Khalil Remtullah amesema timu yake inaendelea na mazoezi pamoja na mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya kujipima kwa ajili ya michuano hiyo yenye ushindani mkubwa.

Remtullaha amesema walitakiwa kuwasili nchini Afrika Kusini mapema ili kuweza kujiandaa na michuano hiyo lakini kutokana na kukosa wadhamini kwa ajili ya kuweka timu kambini kwa kipindi chote kabla ya kuanza michuano hiyo imewalazimu kuondoka nchini siku moja kabla ya kuanza michuano hiyo.