Gofu na raga itakuwa ni sehemu ya michezo itakayoshindaniwa katika Olimpiki ya mwakani na TGU baada ya kuidhinishwa na kamati ya Olimpiki duniani (IOC) kama sehemu ya michezo itakayoshindaniwa.
Na kutokana na hilo, TGU imedhamiria kupeleka timu Brazil.
Michuano hiyo ya Kanda ya 5 ya Afrika itafanyika Kigali, Rwanda baadaye mwaka huu.
Kabla ya kwenda Kigali, TGU inategemewa kuandaa hafla ya kuchangisha fedha mwishoni mwa mwezi wa tatu mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya timu ya taifa.
Uchangishaji fedha pia utafanyika baadaye katikati ya mwaka huu.
Miongoni mwa michuano ya kimataifa ambayo Tanzania inategemewa kushiriki ni pamoja na michuano ya wazi ya Kenya (Kenya Open) na Coast Open itakayofanyika kati ya Februari na Machi, ambayo itakuwa ni kama sehemu ya maandalizi.