Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania TGU Joseph Tango amesema, kwa sasa timu hiyo inaundwa na wachezaji wanne lakini kutokana na ushindani wa michuano ya kanda ya tano wataongezwa nyota wengine wanne ili kutimiza idadi ya wachezaji nane.
Tango amesema, wachezaji hao wataingizwa kwenye kikosi cha timu ya taifa baada ya kumalizika kwa mashindano ya Afrika yatakayofanyika Nairobi nchini Kenya Oktoba 10 mpaka 17 mwaka huu.
Tango amesema, wachezaji watakaounda timu ya wanaume ni Victor Joseph, Abbas Adam, Ally Charo na Isaack Wanyenche ambao kwa sasa wameweka kambi jijini Arusha kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afrika.
Tango amesema, wachezaji wengine wanne kwa upande wa timu ya wanawake wanatarajia kuwachagua katika mashindano mbalimbali ya kitaifa ya Nyerere Masters, Coast Open, Chairman Trophy na Champion yatakayofanyika Dar es salaam, Arusha na Moshi.




