
Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema suala hilo limefikishwa kwa uongozi wa TFF na litatolewa majibu hivi karibuni.
"Msimamo utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa", amesema Alfred Lucas.
Hapo jana Zitto Kabwe ametoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilimanjaro Stars isusie mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biasha ra utumwa.