Ijumaa , 10th Feb , 2017

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limebadili gia angani mara baada ya kuwabadili waamuzi wa michezo ya ligi daraja la kwanza ili kuepusha upangaji matokeo wakati huu ligi hiyo ikielekea ukingoni.

Akizungumza na Kipenga ya EA Radio hii leo, Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema pamoja na uamuzi huo pia wamepeleka waangalizi maalum na wa siri katika michezo yote ikiwemo ya ligi daraja la pili SDL la kwanza FDL na ya ligi kuu VPL.

Msikilize hapa Alfred Lucas akizungumza na Kiberenge wa kipindi cha Kipenga