Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine amesema, Septemba sio mbali hivyo yanatakiwa maandalizi ya kutosha ili kuweza kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika michuano hiyo.
Kwa upande wa Kamati ya Olimpiki nchini TOC, kutoitambua Twiga Stars katika ushiriki wa michuano hiyo, Mwesigwa amesema, TOC na TFF zote zinawakilisha Tanzania hivyo michezo husika inahusika na vyama husika vya michezo hiyo na mashindano hayo kwa ujumla yapo chini ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF.