Jumapili , 9th Nov , 2014

Shirikisho la Soka nchini TFF linatarajia kukutana na wamiliki wa viwanja ili kuweka mpango mkakati wa kuweka miundo mbinu yakutolea maji pindi mvua inaponyesha katika viwanja hivyo.

Akizungumza na East Africa Radio, Mkurugenzi wa Michezo wa TFF, Boniface Wambura amesema viwanja vingi havina miundo mbinu ya kuwezesha kutoa maji ya mvua hivyo kupelekea kusimamishwa kwa mechi kwa muda wa saa 24 pindi mvua inaponyesha.

Wambura amesema kusimama kwa mechi kwa muda huo, inaleta usumbufu kwani kuna baadhi ya mshabiki wamesafiri umbali mrefu kwa ajili ya kuangalia mechi hiyo hivyo kupata gharama za kulala ili kusubiri kumalizika kwa mechi hiyo.