
Kocha wa Tennis walemavu, Riziki Salum
Kocha wa Tenisi walemavu Riziki Salum amesema, wanatarajia kuondoka na jumla ya wachezaji 11 wakiwa ni wakike wanna na saba wakiume.
Riziki amesema,wanaendelea na mazoezi japo bado zipo changamoto ambazo bado zinaendelea kupambana nazo ikiwemo ni pamoja na vifaa ambavyo ni viti vya walemavu ambapo wanachi kimoja huku zikiwa zinatakiwa zaidi ya 10 ili kuweza kuendana na idadi ya wachezaji kwani mpaka sasa wanawachezajia takribani 60.
Riziki amesema, wanaenda kutetea taji ambalo walilichukua mwaka jana lakini bado hawajaweza kupata watu wakuweza kuwasaidia kwa upande wa malazi watakapofika nchini Kenya.
Riziki amesema, iwapo jamii na serikali itaweza kujitokeza na kuisaidia timu itaweza kujiweka katika nafasi nzuri na kuweza hata kupata wachezaji wengi wa hapo baadaye.