Jumatano , 1st Dec , 2021

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania kwa watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ imeifunga Cameroon 5-0 asubuhi ya leo Disemba 1, 2021 na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Afrika kwa wenye Ulemavu 2021 ‘CANAF’.

(Tembo Warrirors walipokuwa wanacheza na Cameroon kwenye CANAF)

Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na Alfan Kyanga dakika ya 2 na 15 , Ramadhan Chomole  dakika ya  18, na Frank Ngailo  dakika ya  36 na  44.

Shangwe na nderemo zilianza pindi tu mchezo huo ulipomalizika kwenye dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam kwa kujua pia kutinga nusu fainali huko kinafanya timu nne hizo kukata tiketi ya kucheza kombe la Dunia nchini Uturuki 2022.

Tembo Warriors wamefuzu hatua hiyo mbele ya Waziri mwenye dhamana ya michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ambaye alikuwa anawaongoza watanzania luishangilia Tembo Warriors ili kuwapa hamasa ya kufanya vizuri zaidi.

Waziri Bashungwa amesem kwa kuhakikisha kwamba Serikali itaendelea kuiisaidia timu  hiyo ili iendelee  kufanya vizuri  kuelekea hatua zinazofuata ikiwemo maandalizi ya Kombe  la Dunia.

Dkt Abbasi Nnae amesema, kwa  kuwa  safari ya kuelekea  kombe la  dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa  kombe  la CANAF linabaki  Tanzania.

Kufuzu huko ni pongezi pia kwa kamati maalum ya kitaifa chini ya katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassani Abbasi ambayo iliisimamia Tembo Warriorsbila kusahau hamasa ya Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu.

Tembo Warriors ilifungwa 1-0 na Uganda, ikapata ushindi wa 2-1 dhidi ya Morocco, Sierraa Leone 1-0 katika hatua ya makundi na hatimaye kuifunga Cameroon 5-0  kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya CANAF.

Mchezo huo pia umeshuhudiwa na Rais wa Mashindano hayo duniani, Mateus Wildack.