Jumanne , 3rd Nov , 2015

Mashindano ya wazi ya mchezo wa Chees yanatarajiwa kuanza kufanyika Novemba 27 mpaka 31 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha nchi zaidi ya tano wanachama wa mchezo huo duniani.

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Chees Tanzania TCA Geofrey Mwanyika amesema, wanatarajia kuwa na wachezaji wengi kutoka nchi mbalimbali ambapo mpaka sasa nchi za Kenya, Uganda, India na Afrika Kusini zimehakiki ushiriki wa mchezo huo.

Mwanyika amesema, kwa upande wa Tanzania, wanamichezo wenye uelewa na mchezo huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya ushiriki wao ili kuweza kuleta changamoto zaidi na kuweza kuutangaza mchezo huo kwa ndani na nje ya nchi.