Ijumaa , 24th Apr , 2015

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania TBF limezitaka klabu za mikoa kuandaa mashindano ifikapo Mei Mosi mwaka huu kwa lengo la kuutangaza mchezo huo.

Akizungumza na East Africa Radio, kamishna wa ufundi na mipango wa TBF, Manase Zablon amesema, mashindano hayo yatafanyika mikoa yote isipokuwa Dar es salaam kutokan a na timu zake kuwa kwenye maandalizi ya ligi ya taifa NBL.

Manase amesema, mashindano hayo yatakuza vipaji vya vijana na kuibua vipaji vipya pamoja na kutumika katika kuchagua kikosi cha timu ya taifa kitakachoshiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.