
Kamishna wa ufundi wa TBF Manase Zabroni amesema, kocha huyo Mathew Mackolister kutoka nchini Marekani ameshasaini mkataba wa miaka miwili lakini watamlipa mwaka mmoja wao kama shirikisho huku mwaka mwingine akilipwa na Serikali atawasili nchini kwa misimu tofauti kwa ajili ya kuweza kutoa mafunzo kwa timu hiyo.
Manase amesema, kocha huyo atawasili nchini April ambapo atakaa nchini mpaka Mei mwaka huu ambapo ataondoka na atarudi tena Septemba mpaka Oktoba mwaka huu ili kuhakikisha anaandaa timu nzuri ya taifa na kuisimamia pamoja na kuwaandaa warithi ambao atasaidiana nao katika kuendesha timu ya taifa.
Manase amesema, kocha Mackolister atafanya ziara mikoani kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachezaji ambao wana vipaji ili kuweza kuandaa wachezaji ambao watakuwa sura ya vipaji vipya vya mchezo huo hapa nchini.