Timu za mpira wa pete zikichuana katika moja ya michuano ya majeshi EA.
Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ litakua mwenyeji wa mzunguko wa nane wa michezo ya majeshi ya ulinzi na utamaduni kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itakayofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 18 hadi 31 mwezi wa nane mwaka huu
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya michezo hiyo brigedia jenerali Cyrile Mhaiki amesema michezo hiyo hufanyika kwa mujibu wa makubaliano ya ushirikiano katika Nyanja ya ulinzi kwa nchini wanachama yaliyosainiwa na wakuu wa nchini wanachama mwaka 2001,
Ambapo lengo kubwa la michuano hiyo ni kuleta ushirikiano, umoja na kufahamiana miongoni mwa majeshi ya nchi hizo,
Na kwakutekeleza hilo mawaziri wa ulinzi kwa nchi hizo wakaazimia kuanzisha michezo hiyo tangu mwaka 2005 ambapo majeshi ya nchi hizo, Uganda, Kenya,Tanzania, Burundi na Rwanda huchuana katika michezo ya soka, netball, kuinua vitu vizito na mbio za nyika
Kwa upande mwingine Brigedia jenerali Cyrile Mhaiki amesema ili kuhakikisha makombe ya michezo yote yanabaki nchini tayari kwa upande wa Tanzania timu za michezo mbalimbali zitakazoshiriki michuano hiyo zimeshaingia kambini kwa maandalizi mazito yakujiandaa na michuano hiyo na hivyo wanauhakika wakutimiza lengo hilo.