Hamis Tambwe akishangilia goli katika moja ya mechi za ligi kuu ya Tanzania Bara iliyomalizika msimu huu.
Kinara wa ufungaji magoli katika ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara wa msimu uliomalizika, Mrundi Hamis Tambwe amesema waamuzi wa Tanzania wanachangia kuvuruga ushindani wa ligi kuu ya Tanzania Bara kutokana na kutowalinda washambulizi mara wanapochezewa rafu kwa kutotoa KADI yoyote hata kama wameumizwa kutokana na rafu hizo.
Akiongea na Muhtasari wa Michezo ya EATV kuhusu ligi iliyomalizika, Tambwe anasema ligi ya Tanzania ni ngumu kutokana na wachezaji kutumia nguvu zaidi ukilinganisha na ligi ya Burundi alipokuwa akicheza awali.
Tambwe amesema Timu za Azam FC na Dar es salaam Young Africans maarufu kama Yanga wamekuwa wakionesha nia ya kumsajili msimu ujao ingawa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Klabu simba, huku akitangaza kukodolea macho timu itakayotangaza kitita kikubwa cha fedha.