Alhamisi , 14th Jul , 2016

Mshambuliaji Amissi Tambwe ameanza mazoezi na kuamsha matumaini ya kuimarisha safu ya ushambulizi ya Yanga kabla ya mchezo wa Jumamosi.

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe

Yanga ina kibarua kizito cha kuivaa Medeama ya Ghana katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tambwe alikuwa akisumbuliwa na Maralia ambapo ameanza mazoezi mepesi na bado anaangaliwa kama atakuwa na uwezo wa kucheza dhidi ya medeama.

Medeama inatarajiwa kuwasili asubuhi ya leo nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Inaonyesha bado Kocha Hans van der Pluijm ana nafasi ya kumtumia ingawa ni kwa asilimia 50 hadi sasa.

Lakini wachezaji majeruhi kama Deus Kaseke aliyepata ajali ya pikipiki, Haji Mwinyi na Geofrey Mwashiuya wanaonekana wataikosa mechi ya Medeama kwa kuwa ni majeruhi na hawakuwa wameanza mazoezi hadi leo.