Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta akiteta na mshambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema anafurahishwa na mazungumzo baina ya uongozi wa klabu hiyo na mshambuliaji wao Pierre-Emerick Aubameyang yanayohusu kurefusha mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo.
Aubameyang raia wa Gabon amekua akihusishwa na kutaka kutimka klabuni hapo huku vilabu vya Real Madrid , Barcelona na PSG vikitajwa kuwania saini ya mshambuliaji huyo.
Arteta amesema kwamba bado anahitaji huduma ya nyota huyo ambaye amekua na mchango mkuwa katika klabu hiyo ambayo inapigania nafasi ya kurejea katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.
TAKWIMU ZA AUBAMEYANG.
-Mechi 83 za EPL ana mabao 52 katika misimu yake miwili ndani ya The Gunners.
-Tangu ajiunge na The Gunners akitokea Borussia Dortmund, Aubameyang amefunga mabao 66 kwenye mashindano yote akiwa na Arsenal,ni Mohamed Salah pekeyake aliyemzidi ambaye alifunga mabao 68 katika mashindano yote tangu ajiunge na Liverpool akitokea AS Roma.
-Raia huyo wa Gabon ndiye kinara wa uzalishaji wa mabao kwa Arsenal msimu huu ambapo amehusika katika mabao 27 katika mashindano yote.




