
Katibu mkuu wa TAHA, Nicolaus Mihayo amesema kuwa mkakati wa chama hicho kwanza ni kuhakikisha mchezo huo unachezwa na ndio maana kwa miaka mingi wamekua wakiandaa na kushiriki michuano mbalimbali nje na ndani ya nchi bila udhamini, japo wamekua wakifanya juhudi kubwa ili kupata udhamini bila mafanikio
Mihayo amesema hata mashindano ya klabu bingwa ya Taifa yanayoendelea hivi sasa, wameamua kufanya katika hali hiyo ngumu kutokana na kuzoea hali hiyo kwa miaka 15 sasa, ingawa hapo kabla walijitahidi kutafuta udhamini kwa kutuma barua za maombi sehemu tofauti lakini cha kusikitisha hawakufanikiwa mpaka wanaanza mashindano hayo.
