Katibu mkuu wa (TAHA), Nicolaus Mihayo amesema kuwa kwa kuanzia kesho kutakuwa na mashindano ya taifa yatakayoanza katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam , na baadae mwezi aprili yatafuata mashindano ya muungano.
Mwezi juni kutakua na mashindano ya shule za sekondari na msingi ambazo kwa bahati zimepata udhamini wa mipira toka chama cha dunia, kitu ambacho kitasaidia michuano ya Umitashmita na Umiseta.
