Jumatatu , 4th Apr , 2022

Klabu ya Simba imethibitisha kuwa nahodha wake, Mohamed Hussein Tshabalala ambaye jana alishindwa kumaliza mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya US Gerndamalie kutokana na kupata maumivu ya misuli anaendelea vizuri na anatarajiwa kusafiri na kikosi kesho kuelekea Tanga ambapo April

Mohamed Hussein''Tshabalala''akishangilia bao.

Tshabalala aliumia katika jitihada za kupora mpira kutoka kwa timu pinzani na akalazimika kuondolewa mnamo kati kati mwa kipindi cha pili na nafasi yake ikachukuliwa na Israel Mwenda.

Akizungumza na East Africa Radio, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba ,Ahmed Ally amesema mashabiki wao wasiwe na wasiwasi kwakuwa beki wao alipata maumivu ya misuli na madaktari walimpatia matibabu na sasa anaendelea vizuri.

Katika hatua nyingine, Ahmed Ally amesema kikosi chao kitaingia kambini jioni ya leo na kinatarajiwa kusafiri kesho kuelekea Mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union utakaochezwa April 7,2022.