Jumatano , 31st Jan , 2024

Mshambuliaji mpya wa Simba, Freddy Michael Koublan amesema ushirikiano kutoka kwa kila mtu ndani ya klabu hiyo itawasaidia malengo ya timu kufika haraka

Koublan ambaye alianza mazoezi na kikosi cha Simba juzi, amesema amefurahi kutua Simba na yupo tayari kuhakikisha anasaidia timu kufanya vizuri katika michezo iliyopo mbele ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara, FA na Ligi ya Mabingwa Afrika

 “Kikubwa ni ushirikiano kutoka kila mtu ndani ya klabu ikiwemo wachezaji wenzangu, nipo tayari kuipambania timu kusaidia kufikia
malengo ambayo yanayotarajiwa”

Ninaimarni kubwa ya kufanya vizuri na kukata kiu ya mashabiki, pia kutowaangusha kocha na viongozi walionisajili ili kufikia kile ambacho wanakitarajia kwenye mashindano mbalimbali yaliyopo mbele yao, amesemma  Freddy

Simba SC ilirejea mazoezini juzi baada ya mapumziko ya siku 10 ambapo timu inajiandaa na urejeo wa ligi kuu na mashindano mengine