Jumanne , 8th Oct , 2024

Sebastien Desabre kaendelea kukiamini kikosi chake kilichopata ushindi dhidi ya Guinea ametaja kikosi cha wachezaji 25 huku Fiston Mayele mshambuliaji wa zamani wa timu ya Yanga na Enock Inonga Baka wakiitwa na kocha huyo kuelekea mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Oktoba 10, 2024

Stars itaondoka majira ya saa 7 usiku leo kwenda Congo DRC kukabiliana na timu ya Congo DRC kwenye mchezo wa kufuzu AFCON 2025 itakayofanyika nchini Morocco Samata ataiongoza Stars huku Congo DRC ikimkosa mshambuliaji wa Brentford ya England Yoane Wissa

Timu ya taifa ya Tanzania itaondoka leo Jumanne Oktoba 8, 2024 majira ya saa 7 kamili usiku  kuelekea nchini Congo DRC kucheza kwenye mchezo wa kufuzu mashindano ya AFCON 2025 yatakayofanyika nchini Morocco. 

Sebastien Desabre kocha wa timu ya taifa ya Congo ametaja  kikosi cha wachezaji 25 ambacho kitashuka dimbani Oktoba 10, 2024 siku ya Alhamisi kukabiliana na taifa Stars. Desabre atawakosa wachezaji wawili Yoane Wissa anayekipiga nchini England kwenye kikosi cha Brentford na Ngal' ayel Mukao ambapo Silas Katompa na William Balikwisha wameziba nafasi zao.

Mbwana Samata atakiongoza kikosi cha Stars kwenye mchezo mgumu ugenini kutokana na ubora wa mpinzani watakayekutana naye siku  ya Alhamisi, Hemed Morocco kaimu kocha kocha wa Tanzania yeye amemuongeza kikosini Ame Ally anayekipiga kwenye timu ya  Mashujaa baada ya nyota wa Simba SC Abdulrazack Hamza kupata majereha kwenye mchezo  dhidi ya Coastal Union.

Stars ilikuatana na Congo DRC kwenye michuano ya AFCON Januari 2024 na mchezo ulitamatika kwa sare,timu hizi zitarudiana Oktoba 15 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam. Kuelekea kucheza michezo ya kufuzu kombe la Dunia 2026,Tanzania itakutana tena Congo DRC hivyo kufanya michezo miwili dhidi ya Matajiri wa Almasi Africa kuwa ni michezo migumu na ya kuvutia.

Taifa Stars inatafuta tiketi ya kufuzu fainali za AFCON kwa mara ya pili mfululizo katika historia yao ambapo kwa sasa  inashika nafasi ya pili kwenye kundi H nyuma ya Congo DRC ambao wanaongoza kundi wakiwa na pointi 6 baada ya kushinda michezo miwili huku Vijana wa Hemed Morocco wakishinda mchezo mmoja na kutoka sare mmoja.