
Kaimu Katibu Mkuu wa RT Ombeni Zavalla amesema, mashindano ya taifa yalikuwa yafanyike Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo waliona hata kama wangerudisha tarehe nyuma bado ilikuwa haiwezekani kwani walipanga kufanya mashindano hayo Juni 03 na 04 mwaka huu ambapo Juni 04 kunamchezo kati ya timu ya Taifa ya Tanzania na Misri.
Kwa upande mwingine Zavalla amesema, wameangalia na wakaona bado kunakipindi cha kuwatengeneza wanariadha kwa ajili ya kufuzu kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki na mwisho ni Juni mwaka huu hivyo wamemua kukaa tena Juni 01 na kupanga tena tarehe nzuri ambayo endapo mwanariadha atafikia viwango vya Olimpiki katika mashindano ya Taifa atakuwa ameongeza idadi ya wachezaji watakaoshiriki Olimpiki Septemba mwaka huu nchini Brazili.