Jumanne , 22nd Jul , 2014

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 2-2 na Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya michuano ya awali yakuwania tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya afrika timu ya taifa ya Tanzania taifa stars inataraji kuingia kambini wiki hii

Kikosi cha stars muda mfupi kabla yakuivaa Msumbiji katika mchezo ulioishia kwa sare ya bao 2-2.

Kikosi cha Taifa Stars kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu) kwenda Mbeya ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji.

Afisa habari wa TFF amesema hayo wakati akitoa shukrani kwa mashabiki waliojitokeza uwanja wa taifa na kuishangilia kwa nguvu timu ya taifa katika mchezo huo ambao uliishia kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2

Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.

Taifa Stars itaondoka nchini Julai 31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto.