Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe.
6 - Ni idadi za assisti alizotoa nyota wa Los Angeles Clippers, Paul George sambamba na alama 41 na rebaundi 13 na kuisaidia timu yake kugaragaza Phoenix Suns kwa alama 116-102 na kuweka hai matumaini ya ubingwa wa ligi ya kikapu nchini Marekani NBA kwa ukanda wa Magharibi kwani wameibuka na ushindi kwenye michezo 2 mfululizo ilhali Suns wameshinda michez 3. Licha ya Suns kupoteza mchezo huo lakini nyota wake, Devin Booker ameendelea kuwa gumzo baada ya kuonesha kiwango safi kwa kupata alama 31, rebaundi 4 na assisti 3 ambazo hazikutosha kuwapa ushindi. Milwaukee Bucks itakipiga na Atlanta Hawks saa 10 Alfajiri ya kesho kwenye mchezo wa mzunguko wa 4 wa fainali ya NBA kwa ukanda wa mashariki.
5 – Ni idadi ya makombe aliyoyatwaa mshambuliaji wa zamani wa Barcelona, Chelsea na timu ya taifa ya Hispania, Pedro Rodriguez kombe la EPL, EUROPA Ligi, UEFA Champions Ligi, Kombe la Dunia na UEFA EUROS na kumfanya kuwa mchezaji pekee Duniani kufanya hivyo rekodi ambayo jana kiungo wa Ufaransa N';golo Kante amekosa fursa ya kuifikia rekodi hiyo baada ya timu yake ya Ufaransa kuondoshwa na Uswizi kwenye 16 bora ya UEFA EUROS.
4 – Ni idadi ya siku zilizosalia kuelekea mchezo wa kariakoo Derby Julai 3, 2021 na tayari tambo na joto kuelekea mchezo huo zimeshika kasi, Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa, bingwa wa ligi kuu bara bado hajapatatikana hivyo wanayanga wasiwe wanyonge kwani wataenda kumfunga mtani wao Simba na wao Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu Kwa upande wa Haji Manara, msemaji wa Simba amesema ule msemo wa kusema mchezo wa watani wa jadi hautabiriki ni msemo wa kizamani, anajiamini kwa kiwango bora alichoonesha Simba kuwa kitawapa ushindi na kupata ubingwa wanne mfululizo mbele ya Yanga. Ikumbukwe kuwa Simba ndiye kinara wa VPL akiwa amecheza michezo 29 na kupata alama 73 ilhali Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 67 na michezo miwili mbele ya Simba ambaye anahitaji alama 4 pekee kufikisha alama 77 ambazo hazitofikiwa na yeye kuwa bingwa.
3 – Ni jumla ya mabao aliyoyafunga Lionel Messi kwenye michuano ya COPA AMERICA msimu huu baada ya alfajiri ya kuamkia leo kufunga mabao 2 kwenye ushindi wa mabao 4-1 ambao timu yake ya Argentina umeipata mbele ya Bolivia na kuwafanya waendelee kuongoza kundi A wakiwa na alama 10 na kufuzu moja kwa moja hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Mchezo mwingine ni ule uliomalizika kwa ushindi wa bao 1-0 kwa timu ya Uruguay kwa pekee lililofungwa na mshambuliaji wake hatari Edinson Cavani 'El Metador' kwa mkwaju wa penalti na kuandika bao lake la pili kwenye michuano hiyo inayoendelea kwenye bara la Amerika ya kusini.
2 – Ni idadi ya ubingwa wa wimbledon kwa msokland Andy Murray ambaye jana alianza vizuri kwenye mzunguko wa kwanza wa michuano mikubwa ya tenis Duniani ya Wimbledon kwa kupata ushindi wa seti 6-4, 5-7 na 6-3 dhidi ya Nikoloz Basilashvili kwenye mzunguko wa kwanza na kuendelea kuweka rekodi ya kutowahi kupokea mchezo wowte wa michuano hiyo kwenye mzunguko wa kwanza. Ushindi huo una maana kubwa kwa Murray ukikumbuka kuwa alikuwa anashindana kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza tokea 2017.
1 – Ni idadi ambayo timu ya taifa ya Uswizi imetinga hatua ya robo fainali katika michuano ya UEFA EUROS na kombe la dunia na hii imekuwa ni kwa mara ya kwanza tokea mwaka 1954 baada ya usiku wa hapo jana kuwaondoa mabingwa watetezi wa kombe la Dunia timu ya Ufaransa kwa ushundi wa penalti 5-4 baada ya sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 120. Sasa, Uwsizi itakipiga dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, timu ya Hispania kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya UEFA EUROS mnamo Julai 2 mwaka huu. Michuano hiyo inatazamiwa kuendelea tena usiku wa leo kwa michezo miwili ya hatua ya 16 bora ambapo England itacheza dhidi ya Ujerumani kwenye mnatange wa kukata na mundu saa 1 usiku ilhali Sweden watachuana na Ukraine saa 4 usiku huku washindi wa mchezo huo watakutana robo.
