Max Verstappen
6. Ni idadi ya pasi za usaidizi za mabao yani Assist alizopiga Raheem Sterling kwenda kwa mshambuliaji Harry Kane kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England ikiwa ni idadi kubwa ya pasi za magoli kutengenezwa na mchezaji mmoja kwenda kwa mchezaji mwingine kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England katika Kalne ya 21.
5. Ni idadi ya ushindi aliopata dereva wa Red Bull raia wa Uholanzi Max Verstappen kwenye mbio za magari Langa langa ama Formula 1 mfululizo baada ya kuibuka mshindi wa mbio za AustriagGP hapo jana na kumfanya kufikisha alama 182 na kutengeneza tofauti ya alama 32 kati yake na Lewis Hamilton dereva wa Mercedes anayeshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Dunia wa mbio hizo.
Mbio nyingi ambazo Max Verstappen ameshinda msimu huu ni zile za Styria, Ufaransa, Monaco na Azerbaijan.
4. Ni idadi sawa ya mabao aliyofunga na pasi za usaidizi wa mabao yani Assists alizotoa mchezaji bora wa Dunia mara sita (6) Lionel Messi kwenye michuano ya Capo America akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina. Idadi hiyo inamfanya Messi kuwa amehusika kwenye mabao 8 kati ya 10 yaliyofungwa na Argentina mpaka sasa kwenye michuano hiyo inayoendela nchini Brazil. Na hizi ni fainali zake za sita anashiriki.
Argentina itashuka tena dimba Julai 7, 2021 kucheza dhidi ya Colombia kwenye mchezo wa nusu fainali.
3. Ni idadi ya miaka aliyosaini Patrick Vieira kuwa kocha wa Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya England akichukua nafasi ya kocha Roy Hodgosn aliyeachana na klabu hiyo mwezi Mei baada ya kutangaza kustaafu. Vieira mwenye umri wa miaka 45 ambaye ni mchezaji wa zamani wa Arsenal na alishinda jumla ya mataji matatu (3) ya Ligi Kuu England akiwa na kikosi hicho na alikuwa nahodha wakati Arsenal inatwaa ubingwa wa mwisho wa Ligi msimu wa 2003-04.
Hiki kinakuwa ni kubarua chake cha tatu kama kocha mkuu baada ya kuvifundisha vilabu vya New York City FC ya Marekani na Nice ya Ufaransa.
2. Ni nafasi anayoshikilia Cameron Norrie kwenye orodha ya wacheza tenisi wa Uingereza kwa upande wa wanaume. Ambapo mchezaji huyo ameashindwa kuweka rekodi yakuwa mchezaji wa pili kutoka uingereza kumfunga Roger Federer.
Hii ni mara baada ya Nurrie kufungwa Seti 3 kwa 1 na mkongwe Federer raia wa Uswis kwenye mchezo uliochezwa masaa 2 na dakika 35 mchezo wa round ya 3 ya michuano ya Wimbledon. Huu unakuwa ushindi wa 13 mfululizo kwa Federer dhidi ya wachezaji wa Uingereza mara ya mwisho kufungwa na mchezaji kutoka taifa hilo ilikuwa 2013 dhidi ya Andy Murray kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya wazi ya Australia.
1. Ni goli pekee lilofungwa na Yanga kwenye mchezo wa derby ya Kariakoo dhidi ya watani zao Simba S.C, goli hilo lilifungwa na kiungo Zawadi Mauya dakika ya 12 ya mchezo. Ushindi huu kwa Yanga unawafanya kuwa wameshinda michezo 38 dhidi ya mnyama Simba kwenye michezo 106 wakati Simba wakiwa wameshinda michezo 31 tu.
Sasa tofauti ya alama kwa timu hizi kwenye msimamo wa ligi ni alama 3, Simba wakiwa vinara na alama 73 wakati Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 70 huku wakiwa wamecheza michezo miwili Zaidi ya Simba wamecheza michezo 32.







