Jumatano , 21st Jul , 2021

Stori sita (6) za michezo (Sports Countdown) leo asubuhi Julai 20, 2021. kwenye Supa Breakfast ya East Africa Radio kuanzia Saa 1:15 Asubuhi, ambapo kila stori inatokana na namba 1 mpaka 6. Na moja ya stori kubwa leo ni PSG wapanda dau kumsajili Pogba na michezo ya Olimpiki yagomewa Japan.

Paul Pogba

6. Ni miezi iliyosalia kabla ya kiungo wa Mancheater United Poul Pogba kuwa huru kufanya mazungumza na klabu zitakazoonyesha nia ya kuhitaji huduma yake, Pogba amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Man United na mpaka sasa hakuna makubaliano yoyote ya mkataba mpya yaliyofanyika, hivyo kufikia mwezi Januari ataruhusiwa kusikiliza ofa za timu zitakazokuwa zinamuhitaji.

Na tayari klabu ya PSG ya Ufaransa inajiandaa kupeleka ofa yakutaka kumsajili kiungo huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28, inaripotiwa PSG watauza baadhi ya wachezaji wao ili kuongeza bajeti ya usajili kwa ajili ya Kumsajili Pogba, ambapo inatajwa kwa sasa wanahitaji kuuza wachezaji ili kufikisha kiasi cha Pauni milioni 50 dau ambalo linatajwa litatumika kama ada ya uhamisho. Na tayari PSG chini ya kocha Mourcio Pochetino imeshafanya usajili wa wachezaji wenye majina makubwa kama Sergio Ramos aliyejiunga akiwa mchezaji huru akitoka reala Madrid, Achraf Hakimi kutoka Inter Milan, Gianluigi Donnarumma kutoka AC Milan, na Georginio Wijnaldum kutoka Liverpool.

 

5. Ni Siku alizopotea Julius Ssekitoleko mwenye umri wa miaka 20 raia wa Uganda huko Japan. Julius ni mwanamichezo kutoka Uganda ambaye alienda Japan kushiriki kwenye michezo ya Olympic kwa watu wanaobeba vitu vizito, lakini alishindwa kufuzu hivyo alipaswa kurudi nchi kwao siku ya Jumanne Julai 20 yani jana lakini kijana huyo alipotea ghafla na kuacha ujembe uliosema hawezi kurudi nchini kwao kwenye maisha magumu anataka kufanya kazi Japan, baada yakutoonekana tangu siku ya ijumaa na akiwa anatafutwa na Polisi hatimaye kijana huyo akijisalimisha kwenye moja ya kituo cha polisi.

Baada ya tukio hilo Rais wa chama cha wabeba vitu vizito Salim Musome amesema watamfuta mchezo huyo kwenye mchezo huo, na kitendo cha wanamichezo kupotelea kwenye nchi za watu sio jambo zuri kwa taifa lao.

 

4. Ni idadi ya mikanda ya uzito wa juu (Heavy weight) anayoshikilia bondia Anthony Joshua na bondia huyo anakibarua cha kutetea mikanda hiyo dhidi ya bondia Oleksandr Usyk raia wa Ukraine, mabondia hao waili watapanda uringo September 25 kuwania mikanda hiyo ya uzito wa juu ambayo ni WBA, WBO, IBFj na IBO.

Pambano hilo litafanyika katika Dimba la Tottenham Hotspur, linalobeba watazamaji elfu sitini, Joshua mwenye umri wa miaka 31 raia wa England mwenye asili ya Nigeria ameshinda mapambano 24 kati ya 25 amepigwa mara moja na mapambano 22 ameshinda kwa KO, wakati mpinzani wake Oleksandr Usyk hajapoteza pambano hata moja kati ya 18 ameshinda yote huku mapambano 13 akishinda kwa KO.

 

3. Ni idadi ya Timu kutoka England zinazomuwania winga wa Bayern Munich Kingsley Coman anayetajwa kuwa na thamani ya Euro milion 90 ambayo ni zaidi ya biliokn 245 kwa pesa za kitanzania.

Vilabu hivyo ni Mabingwa wa England Manchester City ambao wanapambana kuboresha safu yao ya ushambuliaji na kocha wa City Pep Guardiola aliwahi kufanya kalzi na Coman katika klabu ya Bayern Munich kati ya mwaka 2015-2016 , timu nyini Mabingwa wa Ulaya Chelsea ambao wanatajwa wapo tayari kumjumuhisha winga Callum Hudson-Odoi kama sehemu ya ofa ya kumsajili Coman na uongozi wa Chelsea upo kwenye mkakati wa kuhakikishi wanamtimizia kila hitaji kocha Thomas Tuchel, Liverpool ni wababe wengine wanaotajwa kumuhitaji mchezaji huyo wakimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25, kocha Jurgen Klopp inaripotiwa anataka kuongeza ubora kwenye safu yake ya ushambuliaji na kupata mchezaji atakaempa changamoto Sadio Mane.

 

2. Ni idadi ya mabao ya kujifunga aliyofunga Hashmin Musah mlinzi wa klabu ya Inter Allies kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Ghana, mchezo ambao timu yake ilipoteza kwa kufungwa mabao 7-0 na Asante Kotoko, mlinzi huyo amekiri kwamba kwa makusudi alifunga mabao mawili ya kujifunga ili 'kuharibu' mpango wa upangaji wa matokeo ya mechi hiyo.

Musah amesema aliskia Hotelini watu wakipanga matokeo ya mchezo huo iwe 5-1, lakini yeye hakutaka itokee. Na kwenye mchezo huyo mchezaji huyo aliingia akitonea benchi kama mchezaji wa akiba na wakati anaingia tayari timu yake ilikuwa imeshafungwa mabao 5-0, na baada ya kujifunga mabao hayo mawili akatoka uwanjani.

 

1. Ni sawa na idadi ya mwaka umepita tangu mashindano ya Olympic kuhairishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona na sasa michezo hiyo ya Olympic ipo tena matatani kufanyika kutokanana na kamati ya maandalizi ya michuano hiyo nchini Japan kujikuta kwenye shinikizo kubwa la kuahirisha michezo hiyo kutoka kwa wananchi wa Japan ambao wengi wao hawataki michezo hiyo ifanyike nchini mwao wakiwa na hofu huenda kufanyika kwa Olympic kukasababisha wimbi kubwa la maambukizi ya virusi vya Corona.

Mpaka sasa jumla ya visa 71 vya maambukizi vimeripotiwa kutoka kwenye kijiji cha wanamichezo watakao shiriki kwenye michezo hiyo baadhi yao wakiwa wachezaji na wengine ni maafisa walisafiri na timu kutoka mataifa mbalimbali.

Jumla ya wananchi laki moja na arobaini wamesaini maombi kwenda kwa serikali kuomba michezo hiyo isifanyike na tayari wamewasilisha maombi hayo serikalini. Lakini Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Olympic Toshiro Muto amesema michezo hiyo itafanyika kama ilivyopangwa.

Olympic 2020 itaanza siku ya Ijumaa Julai 23 na, ina shirikisha wanamichezo zaidi ya 11238 kutoka kutoka mataifa 206.