Jumatatu , 12th Jul , 2021

Stori sita (6) za michezo (Sports Countdown) leo asubuhi kwenye Supa Breakfast ya East Africa Radio kuanzia Saa 1:15 Asubuhi, ambapo kila stori inatokana na namba 1 mpaka 6. Na moja ya stori ni klabu ya Simba imetwaa ubingwa wa VPL, Italia yaichapa England Fainali Euro 2020.

Timu ya taifa ya Italia wakishangilia ubingwa

6. Ni jumla ya mataji ya Wimbledon aliyoshinda mcheza tennis namba moja Dunia Novak Djokovic raia wa Serbia, Novak amefikisha idadi hiyo ya mataji baada ya kuibuka bingwa wa michuano hiyo kwa kumfunga Matteo Berrettini wa Italia kwenye mchezo wa fainali.

Sasa Djokovic anafikisha jumla ya mataji 20 ya Grandslams na anaungana na Rafael Nadal na Rodger Federer ambao nao wameshinda idadai hiyo ya mataji ya Grandslams. Novak mwenye umri wa miaka 34 ameshinda Grandslams sita (6) kwenye Wimbledon, Australian Open tisa (9), French Open mbili (2) na US Open tatu (3).

5. Ni idadi ya michezo iliyopoteza Coastal Union ya Tanga kwenye michezo 6 ya mwisho ya Ligi kuu Tanzania bara, Coastal ambayo inanolewa na kocha juma mgunda, Imefikia idadi hiyo ya michezo baada ya Kufungwa na Simba Sc mabao 2-0 hapa jana.

Sasa Coastal ina alama 34 ikiwa nafasi ya 17, ikiwa imesalia na michezo miwili kabla ya Ligi kumalizika hivyo wanahitaji kushinda michezo hiyo ili kujitoa katika hatari ya kushuka daraja. Michezo waliosalia nayo ni dhidi ya Mwadui na Kagera sugar.

4. Ni idadi ya Makombe ya Ligi kuu soka Tanzania bara walioshinda Simba SC mfululizo, ambapo hapo jana timu hiyo ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga na kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, hivyo kikosi hicho kutoka mitaa ya Msimbazi ndio mwabingwa wa VPL 2020-21 na ni ubingwa wa nne mfululizo.

Mabao yaliyowapa ubingwa Simba hapa yalifungwa na John Bocco ambaye amefikisha mabao 15 ya Ligi Kuu na ndio kinara kwenye orodha ya wafungaji na Chris Mugalu ambae nae alifunga na lilikuwa bao lake la 13 kwenye VPL.

3. Ni idadi ya penati walizopata timu ya taifa ya Italia kwenye mchezo wa fainali ya Euro 2020 dhidi ya England kwenye changamoto ya mikwaju ya penati na kuibuka mabingwa wa michuano hiyo. Timu hizo zilifikia hatua ya kupigiana penati baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Timu zote zilipiga penati 5, Italy ilikosa mbili na kushinda 3, waliopata Penati kwa Italia ni Domenico Berardi, Leonardo Bonucci na Federico Bernardeschi waliokosa ni Jorginho na Andrea Belotti wakati England walikosa 3 na kupata mbili, waliokosa penati kwa England ni Marcus Rashford, Jadon Soncho na Bukayo Saka na waliopata ni Harry Kanena Harry Maguire. Huu ni Ubingwa wa pili wa Euro kwa Italia na wa kwanza tangu 1968.

2. Ni nafasi wanayoshikilia klabu ya Yanga kwenye msimamo wa Ligi kuu VPL, ambapo tafiti zinaonyesha timu hiyo itakusanya taklibani bilioni 11 msimu ujao kutoka katika vyanzo mbali mbali vya fedha vya klabu hiyo.

Yanga imeteka vichwa vya Habari baada ya kusaini mkataba wa udhamini na Azam TV wa miaka 10 wenye thamani ya bilioni 41, na inaripotiwa kuwa Yanga itatengeneza taklibani bilioni 8 kutoka kwenye mikataba ya udhamini pekee yake hivyo wakikusanya na pesa kutoka kwenye vyanzo vingine kama ada za uanachama na match day activities inakadiliwa kufikia dau hilo.

1. Ni ushindi pekee uliopata timu za taifa za mpira wa kikapu za Afrika dhidi ya timu ya taifa ya Marekani, ambapo Timu ya taifa ya Nigeria imekuwa timu ya kwanza kutoka barani Afrika kushinda mchezo dhidi ya Marekani katika historia ya mchezo wa mpira wa kikapu.

Wameweka rekodi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa alama 98 kwa 90 kwenye mchezo wa kirafiki Uliochezwa Las Vegas ambao ni wamaandalizi kuelekea michuano ya Olympic.