Gareth Southgate ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Uingereza wenye umri chini ya miaka 21.
Mtendaji mkuu wa FA Martin Glenn,amesema kuwa kupatikana kwa kocha mpya kunaweza kuchukua miezi kadhaa, huku pia akimtaja meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake kama moja ya chaguo lao.
Glenn amesema kuwa ingawa Southgate atakuwa kocha wa muda bado ana nafasi ya kupewa mikoba ya kuwa kocha mkuu wa timu hiyo lakini bado watafanya mchakato wa kuhakikisha wanapata mrithi sahihi wa Roy Hogson aliyeng'atuka hivi karibuni.
Roy Hodgson alijiuzulu baada ya kukifundisha kikosi cha England kwa miaka mitatu kufuatia kichapo dhidi ya timu ndogo ya Iceland mjini Nice siku ya Jumatatu na kutupwa nje ya mashindano ya mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa.


