Jumamosi , 17th Feb , 2018

Klabu ya soka ya Simba jioni hii imethibitisha kuwa kesho itasafiri kuelekea nchini Djibouti kwaajili ya mchezo wake wa marejeano dhidi ya wenyeji wao Gendarmerie kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kupitia kwa taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya klabu hiyo imeeleza kuwa kikosi cha Simba kimefanya mazoezi ya mwisho jioni ya leo tayari kwa safari ya kwenda kusaka tiketi ya kutinga hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Simba ambayo ilishinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam inahitaji sare tu au isifungwe zaidi ya mabao manne ili kuvuka hatua hiyo ya awali ya michuano hiyo.

Kikosi cha Simba ambao ndio vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara kinatarajiwa kuondoka nchini majira ya saa 11:00 jioni siku ya kesho ambapo mchezo wao unatarajiwa kupigwa Februari 21.