Kikosi cha wekundu wa msimbasi Simba katika picha ya pamoja kabla ya moja ya mechi ya ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Ajibu aliyeingia akitokea benchi alionyesha umahiri mkubwa kwenye mechi hiyo ambayo kocha Dyran Kerr alitumia wachezaji saba wa kimataifa ambao hata hivyo hawakuweza kuonyesha kiwango cha kulidhisha.
Ushindi wa Simba unawaongezea pointi tatu muhimu na kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo kwa sasa imekwea mpaka nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 27 sawa na Mtibwa Sugar lakini wanaipiku kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Wekundu hao wa msimbazi wanatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki kwenye michuano ya Mapinduzi ambapo wao ndio mabingwa watetezi wa michuano.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>