Wachezaji wa Simba
Simba amefanikiwa kupata tiketi hiyo baada ya kumfunga Azam bao 1-0 katika fainali ya pili iliyofanyika katika uwanja wa Majimaji Songea, kwa goli la jioni kabisa dakika 89 lililofungwa na Luis Miquissone kufuatia faulo ya haraka iliyopigwa na Bernard Morrison.
Goli lililoibua mjadala mkubwa kutoka kwa mashabiki wa soka pande mbalimbali za nchi, wapo walioamini halikustahili kuwa goli kwa sababu mwamuzi hakupiga filimbi kuruhusu pigo kufanyika , wapo walioamini kuwa ni goli sahihi halina dosari yeyote.
Awali wapinzani wao wakuu Yanga, walitangulia kwenye fainali hiyo baada ya kuifunga Biashara Mara bao 1-0 katika fainali ya kwanza iliyofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora siku ya ijumaa.
Bingwa wa michuano hii atawakilisha nchi kwenye mashindano ya kombe la shirikisho CAF kwa msimu wa 2021/2022.
Hii si mara ya kwanza kwa Simba na Yanga kukutana nje ya Dar-es-Salaam, wameshakutana mara kadhaa katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Morogoro huu utakuwa mchezo wa 3 ndani ya mwaka huu kukutana ,awali walikutana januari 13 kwenye mapinduzi cup Zanzibar na wanatarajiwa kukutana katika mchezo wa pili wa ligi kuu julai 3 2020 uwanja wa Benjamin Mkapa.
Takwimu za mechi rasmi za watani wa jadi Simba na Yanga tangu mwak a 1965 ,wamekutana mara 107 Yanga amepata ushindi mara 37 huku Simba akishinda mara 32 sare zikiwa 38.



