Shomari Kapombe wakati akiwa kwenye matibabu Afrika Kusini
Taarifa ya Simba iliyotolewa leo, Machi 5, 2019, inaeleza kuwa Kapombe ambaye amekuwa nje ya uwanja tangu Novemba mwaka 2018, atarejeshwa Afrika Kusini muda wowote kwaajili ya vipimo vya mwisho.
''Shomari Kapombe anatarajiwa kurejea Afrika Kusini wiki hii kwa ajili ya vipimo vya mwisho kabla ya kuruhusiwa kuanza mazoezi mepesi. Pichani Kapombe akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Crescentius Magori'', amesema.
Mlinzi huyo wa kulia wa Simba aliumiwa mguu akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania wakati ikijiandaa na mchezo wake wa Kundi L dhidi ya Lesotho katika kuwaniwa kufuzu AFCON 2019.
