Jumatano , 15th Mar , 2023

Mabingwa Watetezi wa Kombe la Shirikishso Tanzania Bara ‘ASFC’ Young Africans wamepangwa kucheza dhidi ya Geita Gold FC katika mchezo wa Robo Fainali ya Michuano hiyo msimu huu 2022/23

Young Africans ambayo ilitwaa ubingwa wa michauno hiyo msimu uliopita kwa kuifunga Coastal Union kwa changamoto ya mikwaju ya Penati baada ya sare ya 3-3 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid-Arusha, itacheza mchezo huo wa Robo Fainali nyumbani jijini Dar es salaam.

Geita Gold FC watakuwa na kazi kubwa ya kulipa kisasi dhidi ya Wananchi, hasa ikizingatiwa mwishoni mwa juma lililopita ilikubali kichapo cha 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mbali na mchezo huo wa Ligi Kuu, Geita Gold FC itakuwa inakumbuka mchezo wa Robo Fainali wa ‘ASFC’ dhidi ya Young Africans uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam msimu uliopita 2021/22. Mchezo huo ulishuhudia Geita Gold FC ikipoteza kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.

Michezo mingine ya Robo Fainali ya ASFC iliyopangwa leo Jumatano (Machi 15) kupitia Droo iliyofanyika Studio za Azam Media jijini Dar es salaam.

Simba SC Ihefu SC

Singida Big Stars Mbeya City

Azam FC Mtibwa Sugar