Jumatatu , 4th Apr , 2022

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika Simba SC itajua hatma yake ya kumjua mpinzani watakae kutana nae kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hii. Droo ya robo fainali ya kombe la shirikisho inafanyika kesho Aprili 5, 2022 Cairo Misri.

Kikosi cha Simba SC

Simba imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi D wakiwa na alama 10 sawa na vinara wa kundi hilo RS Berkane. Simba ilifikisha alama hizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya us Gendermerie kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

Katika droo ya kesho ya kupanga michezo ya hatua ya robo fainali itakayofanyika makao makuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF huku Cairo nchini misri, Simba inaweza kupangwa na kinara wa kundi A,B au C. timu hizo ni Al-Ahli Sports Club ya Libya, TP Mazembe ya DRCongo na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Katika hatua hii timu zilizokuwa kundi moja haziwezi kukutana lakini zile zinazotoka kwenye nchi moja zinaweza kupangwa kucheza kwenye hatua hii.